Mpelelezi nguli wa Afrika, Willy Gamba, hakosi panapokuwa na mapambano kati ya upande wenye haki, upande wa umma na ule wa dhuluma. Kwa kushirikiana na wapelelezi mahiri kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kwa kutumia medani za kivita, mateke, ngumi, kung fu achilia mbali bastola, visu na silaha nyingine wanapambana dhidi ya Makaburu hao na vikundi mbalimbali vya kigaidi vilivyoshirikiana nao. Hekaheka zinatokea Arusha, Makaburu wanakipata cha moto. Mwindaji awa mwindwaji…fuatilia.




