BWENI LA WASICHANA

TSH 22,000

Availability: In stock

SKU : 978-9987753840
Category:

Usiku huo nilikuwa nasimamia maandalizi ya masomo ya usiku. Nikapigiwa simu na Rose, nikaipokea. Wakati naongea naye, nikawa natembea taratibu kama naelekea kwenye mabweni. Ghafla, nikaona taa za bweni wanalolala “Buibui” zinawaka na kuzima, nikajua ni hitilafu katika mfumo wa umeme. Nikataka kusogea ili nithibitishe kisha nitoe taarifa mapema kwa uongozi na matengenezo yafanyike. Nilisogea mpaka mlangoni, taa zikawaka moja kwa moja, na kwa kuwa kulikuwa na dalili za kuwemo mwanafunzi, nilitaka kujua kwanini hayupo darasani wakati wenzake wote walikuwa wana-jisomea. Nilingia nikakuta hali ya ukimya sana, nikatembea mpaka karibu na mwisho wa bweni, nilichokiona ni aibu kubwa! Huwezi amini, “Buibui” waliponiona wakadondosha khanga! Wakabaki kama walivyozaliwa..

Shopping Cart
Scroll to Top
preloader