Kitabu hiki kimekusanya simulizi za kubuni zenye asili ya Kiarabu, Kiajemi na Kihindi, zilizotafsiriwa na Hassan Adam kwa Kiswahili cha kisasa. Kinaendeleza hadithi za kusisimua za mapenzi, uchawi, ujanja, safari, na maadili mbalimbali ambazo husimuliwa na Shahrazade kwa Mfalme Shahryar.




